Karibuni!

Eröffnung Behindertenschule
Mrimbo Uuwo

Inaunganisha ushirikiano

 

Tangu mwaka 1985, ikiwa ni: Ev. -Luth. Parokia Heikendorf katika Schleswig-Holstein na Mrimbo nchini Tanzania.

 

 

 

Ushirikiano unamaanisha Kujifunza, Kuelewa, Kuheshimu, Kuvumilia, Kusaidia, Kushirikiana, Kusuluisha, Kuaminiana, Kusali na kufanya kazi kwa pamoja….
Inasisimua kuwa kwenye ushirikiano na mbadilishano na watu ambao wanatoka katika mazingira, tamaduni na mila tofauti kabisa. Inakupa nafasi ya kutafakari na kutathimini maisha yako mwenyewe, vipaumbele na imani.

Washirika wote katika uhusiano huu wanapata motisha mpya na wanahamasishwa kufanya mabadiliko ya kudumu katika maisha yao wenyewe.
Sio bahati mbaya kuwa kwenye uhusiano na sharika ndani ya moja ya nchi maskini zaidi duniani. Kikundi ncha Heikendorf nchini Tanzania kina takribani wanachama 15 wanaume na wanawake ambao wanajitoa na hawafurahii umaskini uliokithiri na mabadiliko ya kusuasua katika nchi za dunia ya tatu.
Tunasukumwa na maono ya dunia ambayo inampa kila mtu chakula cha kutosha, huduma bora za afya na elimu bora. Ambapo sisi katika timu ya pamoja tunapigania maendeleo endelevu, usawa wa haki na amani. Dunia ambayo uumbaji wa Mungu unatunzwa na kuendelezwa. Inatufanya tujisikie vyema kwa kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kuhimiza usimamizi mzuri na usawa duniani.

Tunapendezwa kuwasaidia washirika wetu waliopo Mrimbo katika miradi yao ya kijamii. Watu wengi bado wana nafasi ndogo ya kupata elimu ya juu, uchaguzi wa ajira, kipato cha kuwaida, mazingira salama ya kuishi, usalama wa jamii au uhuru wa mtu binafsi. Msaada wetu unalenga kuwawezesha kugundua na kuendeleza uwezo wao wenyewe.