Ausbildung

Kiumo Vocational Training Centre

ausbildung

KITUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI KIUMO – KVTC
Elimu na mafunzo ni muhimu kwa maisha huru naya kijitegemea. Hufungua milango ya kuondokana na umaskini pamoja na maisha ya utegemezi wa misaada. Elimu inaweza kupunguza na kuepusha kujiingiza katika uzembe, uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya.
Kikiwa kama moja ya miradi ya pamoja ya ushirikiano, kituo hiki cha mafunzo ya ufundi kwa wahitimu wa shule za msingi kilianzishwa. Tangu mwaka 1992, tumekuwa tukitoa elimu na kufundisha katika idaza za

  •  Useremala
  •  Ushonaji wa nguo
  •  Mafunzo ya Uhazili pamoja na Upigaji-chapa(Typewriting)
  •  Na kozi za Kompyuta

Tangu wakati huo takribani vijana 650 wasichana na wavulana wamehitimu mafunzo KIUMO na kutunukiwa vyeti rasmi vinavyotambulika kisheria. Kituo hiki cha mafunzo ni mradi wa Kidiakonia, ambao unatoa udhamini kwa yatima, kwa wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu na hata kuwasaidia wanaoshindwa kulipa ada zao. Baada ya mitihani wanafunzi hupewa vifaa ambavyo vinawawezesha kujiajiri wenyewe au kujifunza zaidi.
KIUMO inajumuisha pia Kitengo cha Uzalishaji ambacho huchangia fedha za uendeshaji pamoja na mafunzo kwa vitendo. Ushonaji huzalisha mavazi kwa mahitaji maalumu kama vile sare za shule. Kitengo cha Useremala huunda na kuzalisha madirisha, milango na samani zenye ubora wa juu. Kutokana na upungufu wa miti ya mbao(Ambapo mkoni Kilimanjaro ukataji na uvunaji wa miti ya mbao umepigwa marufuku) na gharama za juu,utumiaji wa mbao na chuma kwa pamoja hufanywa. Wanafunzi waliohitimu pia wanaweza kuajiriwa katika karakana ya useremala kuendana na mahitaji ya kazi au wanaweza kutumia vifaa na vitendea kazi vilivyopo kwa kazi zao binafsi nyakati za machana baada ya muda wa masomo. Ajira 10 hadi 12 zimepatikana Mrimbo kupitia KIUMO-VTC
Msaada kutoka Heikendorf: Shule inapaswa kujitahidi ili kuondokana na utegemezi wa misaada lakini hata hivyo bado kiasi cha msaada kinahitajika kutoka Heikendorf. Kimsingi, ni kwa ajili ya Uwekezaji, Ukarabati, Matengenezo ya mashine pamoja na vifaa ikiwemo vya wahitimu. Mshaara wa Meneja, ambaye KIUMO inajivunia pia unategemewa kutoka Heikendorf.
Maendeleo ya baadae: Lengo ni kuwaelimisha na kuwafundisha vijana wadogo taaluma zenye uhitaji mkubwa wa baadae, hivyo kiwango na ubora wa elimu unapaswa kuwa wa kudumu. Taaluma mbili zaidi zimeanza kutolewa tangu mwaka 2016, ambazo ni;

  •  Ufundi wa kuchomelea(Ulehemu)
  •  Na Ufundi Umeme

Mwaka 2014, jendo jipya la shule kwa ajili ya mafunzo ya nadharia lilizinduliwa kwa msaada wa Bingo Projektförderung na Bread for the World. Hii inafungua fursa mpya kwa maendeleo zaidi ya kituo hiki cha mafunzo ya ufundi. Wakati wa ziara yetu mwezi Machi mwaka 2016, tulikubaliana kwenye shughuli endelevu kadhaa za mafunzo na uzalishaji ikiwemo mradi wa kukausha mbao. Elimu ya Ufundi haina tena mvuto kwa wanafunzi nchini Tanzania ambao mara nyingi huwa na mawazo yasiyo na uhalisia kuhusu soko la ajira. Ili kukidhi mahitaji ya masoko kozi mpya za ufundi zilizotajwa hapo juu zilianzishwa. Kwa mipango ya baadae tungependa kuanzisha nishati ya mionzi ya jua kwa uzalishaji wa nishati salama na mbadala.
Ushirika na Mahusiano: Ushirikiano wetu ulianza tangu mwaka 1985. Sharika za Makanisa ya Kiinjili ya Kilutheri ya Heikendorf, Schleswig-Holstein nchini Ujerumani na Mrimbo, Mwika nchini Tanzania, Afrika.

Neubau des Schulgebäudes für Kiumo

Kiumo Vocational Training Center Uuwo, Foto: Minja