kuhusu sisi

Kutuhusu sisi: Kikundi cha Tanzania (The Tanzania Group)

 

Sitzung Tansaniagruppe Heikendorf

Heikendorf ni kijiji kidogo chenye wakazi takribani 8,000 kilichopo kwenye fjord nzuri ya Kiel.
Sharika za kilutheri za Heikendorf na za Mrimbo, Tanzania zimekuwa pamoja tangu mwaka 1985. Kikundi cha Tanzania (The Tanzania Group) hapa Heikendorf kina wanachama takribani 15 wanaume na wanawake ambao wana msukumo mkubwa kwa Afrika na wangependa kuchangia zaidi katika usawa wa dunia. Ni sababu hii inatufanya tuendeleze kazi ya Helmut na Doris Krieg ambao walianzisha ushirikiano na kuweka muhuri wao kwa miaka mingi kwa kipaji na umahiri mkubwa. Kila Alhamisi ya tatu ya kila mwezi tunakutana katika nyumba ya usharika kupata habari mpya kutoka Mrimbo pamoja na kuanzisha mawazo mapya na kujadili miradi iliyopo. Tunapitia mawazo yetu na kuyahusisha na maisha nchini Tanzania. Tunakusanya michango, kuendesha matukio ya uchangishaji fedha, na kukusanya fedha kutoka kwa wahisani nje ya washirika. Hii inatuwezesha kusaidia miradi ya kijamii Mrimbo ambayo vinginevyo isingewezekana wala kuwepo.
Juu ya yote, tunawekeza katika elimu kwa sababu elimu bora ni msingi wa maendeleo huru ya Tanzania. Shughuli zetu zinajumuisha uwasilishaji wa taarifa, uonyeshaji wa picha, machapisho pamoja na taarifa kwa vyombo vya habari. Tunasheherekea siku ya Tanzania mara moja kwa mwaka ndani ya kanisa. Tuna mawasiliano ya karibu naya kila mara na washirika wetu Mrimbo. Tunasafiri mara kwa mara kwenda Tanzania na tunawakaribisha wageni kutoka Tanzania kuja Heikendorf. Tuna mtandao mpana wa mawasiliano na tunatumia kila nafasi kujifunza. Kutokana na ushirikiano huu, ushirika zaidi umeendelea kukua kwa miaka mingi.
Je ungependa kushiriki? Tunatafuta vipaji mbalimbali: Wahandisi, Wakulima, Wachumi, Mafundi Seremala, Mafundi Cherehani(Washonaji), Watangazaji, Wataalamu wa nishati ya mionzi ya jua, Waalimu wa elimu na makundi maalumu, Wataalamu wa afya, Wataalamu na wajuzi wa mitandao, Wataalamu wa Afrika au hata wewe tu!
Hakuna awezaye kuyafuta machozi ya mwezie bila kulowesha mikono yake! (Afrika)